22 Desemba 2019 - 08:10
Macron ataka kusitishwa migomo nchini Ufaransa

Rais wa Ufaransa amewataka wafanya maandamano nchini humo kusitisha migomo katika sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya.

(ABNA24.com) Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na Rais wa Kodivaa huko Yamoussoukro mji mkuu wa nchi hiyo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amewataka wafanya maandamano nchini kwake kusitisha migomo katika sherehe za mwaka mpya na kufikia mapatano ya muda.

Maelfu ya walimu, wafanyakazi wa sekta ya reli na wa hospitali wa nchini Ufaransa walianza kufanya migomo tangu Disemba 5 mwaka huu kulalamikia mpango wa Rais Macron wa kufanyia marekebisho mfumo wa wastaafu. Migomo hiyo inatajwa kuwa moja ya migomo mikubwa zaidi ya uuma nchini Ufaransa katika miongo ya karibuni.  

Hadi kufikia sasa watu zaidi ya 11 wameuawa na karibu elfu 14 wamejeruhiwa au kutiwa mbaroni katika maandamano hayo nchini Ufaransa. Awali maandamano hayo yalianza kupinga siasa za uchumi za serikali ya Rais Emmanuel Macron khususan katika sekta ya petroli na tozo za kodi hata hivyo maandamano hayo yalishtadi haraka na kuchukua mkondo wa kisiasa.  

Utafiti wa maoni uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Odoxa unaonyesha kuwa robo tatu ya wananchi wa Ufaransa hawaridhishwi na utendaji wa Macron.

..........
340